Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, limepata pigo baada ya Askari wake kuuawa na kundi la waasi kwenye nchi Jamhuri ya Afrika ya kati.
Askari huyo aliyekuwepo kwenye kikosi cha askari wanaolinda amani kwenye nchi hiyo ambapoa Kanali Ramadhani Dogoli, Msemaji wa Jeshi hilo amesema tukio hilo limeyokea Juni 3,mwaka huu majira ya 10: 30 jioni. Waasi hao walishambulia askari 90 walipokuwa kwenye majukumu yao ya kulinda amani.
Ameeleza kuwa utaratibu wa kuurudisha mwili wa askari aliyefariki kuja nchini unafanywa na Umoja wa Mataifa ambapo wengine 18 wamejeruhiwa na watano ambao hali zao sio nzuri wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Kanda ya Umoja wa Mataifa iliyopo mji wa Bangui.
