Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 nchini (Ngorongoro Heroes) itacheza na timu ya Taifa ya Mali kwa vijana chini ya Umri wa miaka 20 Jumapili Mei 13,2018 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa Ngorongoro Heroes wapo kambini wakiendelea kujifua na mchezo huo, ili kuwakabili vyema vijana wa mali na kesho watafanya vipindi viwili vya mazoezi yaani asubuhi na jioni .
Taarifa za ndani kutoka kwa mkufunzi mkuu wa Timu hiyo Ammy Ninje,amethibitisha kumuacha mlinda mlango nambari moja wa timu hiyo Ramadhani kabwili,ambae ameondoka kuelekea Algria na klabu yake ya yanga kuvaana vikali na USM Alger katika kombe za shirikisho barani Afrika
Kikosi hicho hakina majeruhi vijana wana morali kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu fainali za vijana Africa.
Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10 jioni na kiingilio katika mchezo huo ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa VIP na kwa viti vya Mzunguko ni shilingi elfu moja (1,000).
