Ajisalimisha Polisi baada ya mzigo alioiba kung'ang'ania kichwani





Kijana Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha Kituo cha Polisi baada ya mzigo wa Mahindi (Kg 20) anaodaiwa kuuiba kung'ang'ania kichwani.
Kijana huyo ameeleza kuwa mzigo huo aliuiba kwa Mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi mkoani Pwani na kuongeza kuwa alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi ili auache kwa mwenzake kisha arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling'ang'ania kichwani.
                
Baada ya jitihada nyingi za kuutoa kichwani pamoja na kuzunguka nao kwa muda mrefu, amedai kuwa alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha Polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.

Post a Comment

Previous Post Next Post