Ajirusha kutoka juu ya Msikiti wa Makkah , afariki


Mwanamume mmoja ambaye uraia wake haujajulikana, amejirusha kutoka juu ya Msikiti wa Makkah, Saudia hadi chini na kufariki papo hapo. 
Tukio hilo limetokea Ijumaa (jana) usiku wa saa 9:20 Makkah. Taarifa zaidi zilizoandikwa na mtandao wa gulfnwes zinaeleza kuwa, mwanamume huyo aliruka kwa kupitia uzio uliwekwa kwa ajili ya usalama wa waumini wanaokwenda kwenye msikiti huo kwa ajili ya ibada ya Hijja na zingine.

Mtu huyo alifariki papohapo kutokana na kugonga chini sehemu iliyo ngumu. Polisi wa Saudia wameeleza kuwa mwili wake umepelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi sambamba na kutaka kujua nchi aliyotoka.

Post a Comment

Previous Post Next Post