Klabu ya Soka ya Yanga imefanya mabadiliko kwa kuunda kamati maalumu kwa ajili ya mikakati ya kuisuka upya timu hiyo
Katika wake ulifanyika leo Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, Yanga imetangaza kamati maalumu ya kwa ajili kuimarisha timu hiyo
kamati hiyo iliyoridhiwa na mkutano huo imeundwa na watu 12 ikiongozwa na Mwenyekiti Tarimba Abbas na Makamu Mwenyekiti Said Mecky Sadick, wajumbe wengine ni Ridhiwan Kikwete,Hussein Ndama,Hamad Islam.
wengine ni pamoja na Abdallah Binkleb, Nyika Hussein, Samwel Lukumay, Mashauri Lucas, Yusuphed Mhandeni, Makaga Yanga, Majid Suleiman
Wakati huo klabu hiyo imeunda Bodi mpya ya wadhaamini inayoundwa na waliokuwepo awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) George Mkuchika mke wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, Jaji Mstaafu John Mkwawa pamoja na Mzee Katundu.
