Mechi za marudiano michuano ya Europa League zitachezwa usiku wa leo ambapo Arsenal watakuwa ugenini nchini Hispania kuvaana na Atletico Madrid.
Timu hizo mbili katika mechi ya kwanza zilitoka sare ya bao 1-1.
Mchezo mwingine wa leo ni wenyeji Salzburg ya Austaria watakao pambana vikali dhidi ya Marseille ya Ufaransa ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa awali.
Timu mbili zitakazofanikiwa kufuzu baada ya mechi za leo, zitakutana kwenye fainali za michuano hiyo itakayofanyika Mei 16 nchini Ufaransa.