Mgunduzi wa Tanzanite alamba Mil 100 kutoka kwa JPM

Rais John Magufuli ametoa ahadi ya kumpatia mgunduzi wa madini ya Tanzanite, Jumanne Ngoma Milioni 100 kwa ajili ga kumsaidia kujikimu na matibabu baada ya mzee huyo kupooza mguu.
Magufuli ametoa ahadi hiyo leo wakati akizindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite, yaliyopo eneo la Mererani, kaskazini mwa Tanzania uliojengwa kwa lengo la kuzuia wachimbaji madini kukwepa kulipia ushuru na kuiba madini.
 "Leo tusingekuwa tunazungumza Tanzanite kusingekuwa na huyu Baba Jumanne Ngoma, leo anaumwa mguu wake umepalalaizi ili kusudi aende akatibiwe vizuri serikali yangu italipa Shilingi Milioni 100' amesema Rais Magufuli.
Ngoma alivumbua aina hiyo ya madini ya Tanzanite mwaka 1967 madini ambayo ni ya kipekee kwa Tanzania na hayapatikani sehemu nyingine yeyote duniani.
Mauzo ya Tanzanite duniani yanafikia dola za Marekani milioni 50.

Post a Comment

Previous Post Next Post