Hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa la utapeli kupitia simu za mkononi kwa njia ya ujumbe mfupi wanajifanya waganga watatuzi wa shida za binaadamu.
Leo Juni 6 Jeshi la Polisi nchini kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Barnabas Mwakalukwa limekemea vikali utapeli huo unaofanywa kwa njia .
Taarifa hiyo imebainisha kuwa utapeli huo umekuwa ukifanywa na watu wanaojifanya waganga wa kienyeji wanakutaka utume hela ili ufanikiwe au akutatulie matatizo.
Amesema kuwa kitengo cha jeshi hilo cha uhalifu wa mitandaoni kinaendelea na upelelezi na wahalifu watafikishwa kwenye mikono ya sheria.


