Tetesi za usajili:Kibarua cha Conte chaota nyasi Chelsea yapanga na Blanc wa PSG , Man u Liver mipango yao hii


Chelsea inakaribia kumsajili aliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc kuchukua mahala pake Antonio Conte. (Express)

Manchester United wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili beki wa Sevilla Clement Lenglet, 22.

Raia huyo wa Ufaransa ana kifungu cha kandarasi yake kitakachogharimu £30.7m ili kuondoka katika klabu hiyo. (L'Equipe - in French)

Liverpool inapanga dau la £10m kumnunua winga wa Nigeria mwenye umri wa miaka 22 Moses Simon kutoka klabu ya Gent. (Liverpool Echo)

Leicester inaongoza katika kumsajili kiungo wa kati wa Norwich James Maddison, 21, huku klabu hiyo ikitaka kupewa zaidi ya £20m ili kumuuza raia huyo wa Uingereza. (PA)

Leicester imeanzisha mazungumzo ya kutaka kumsaini beki wa Ireland kaskazini Jonny Evans, 30, ambaye anapatikana kwa dau la £3m baada ya kushushwa daraja na klabu ya West Brom. (Mirror)àaà

Post a Comment

Previous Post Next Post