Kauli 5 za Rais Magufuli kuhusu nyongeza ya mishahara



Rais Magufuli leo Mei 1, 2018 amehutubia taifa katika sherehe za kuadhimisha Siku Kuu ya Wafanyakazi ambayo kitaifa ufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 1 mwezi Mei ambapo kwa mwaka 2018 kitaifa yamefanyika mkoani Iringa.

Katika hotuba yake Rais Magufuli ametoa kauli mbalimbali zinazohusu kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma ambapo kauli zifuatazo ni miongoni mwa hotuba yake hiyo.
 
1. Hata mimi ninapenda kupandishiwa mshahara, hata spika Ndugai anapenda lakini kwa halisi ya sasa hivi lazima niwaeleze ukweli (hakuna nyongeza ya mshahara).

2. Ningekuwa na hela kwenye chungu zimebaki, leo ningetamka tu kuwa mpewe hela, ila nikitamka nitawapa nini?

3. Najenga Stigler's gorge, kwangu hiyo ni muhimu zaidi kuliko kuzichukua hizi trilioni 3 kuzipeleka kwenye mishahara ya wafanyakazi. Kwangu mimi miradi hii ni muhimu kuliko kupandisha mishahara.

4. Nilitamani sana mwaka huu kupandisha mishahara ila baada ya hizi changamoto nyingi nikaona kwanza tuzimalize. Huo ndio ukweli na ninaomba mnielewe. Napenda niwahakikishie wafanyakazi wote nchini kwamba serikali yangu inawathamini sana ndio maana inawaambia ukweli.

5. Kipindi changu cha Urais hakitaisha bila kupandisha mshahara, na kupandisha kwangu haitakuwa elfu kumi, nitapandisha kweli kweli. Nawahakikishia sitawasahau.


Post a Comment

Previous Post Next Post