Huyu ndiye muigizaji wa vichekesho ambaye Gabo amemvulia kofia


Nyota wa filamu za bongo movie, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amemtaja msanii ambaye anamkubali katika tasnia ya uchekeshaji.

Gabo amesema katika wachekeshaji anaowakubali zaidi, Rashid Mwinshehe 'Kigwendu' ni namba moja japo kuna wengi ambao wanaofanya vizuri katika tansia hiyo ya kuchekesha.

Gabo amesema Kigwendu ni mchekeshaji mahili sana na mwenye uwezo mkubwa wa kubuni vitu mbalimbali kwenye kazi yake ya kuchekesha.

“Kigwendu ni mchekeshaji mzuri wenye umakini kubwa kwenye kazi zake katika waigizaji wanaochekesha basi kura yangu inamdondokea yeye.

“Wasanii tunapaswa kuwa wabunifu kwani hapa Tanzania kuna waigizaji wenye vipaji vikubwa tukishirikiana kwa pamoja tunafika mbali kama nchi zingine kupitia filamu,” amesema Gabo.

Post a Comment

Previous Post Next Post