Ndoa ya Alli kiba na Abdu Kiba yamkuna Christian Bella

Nyota wa muziki wa bongo fleva, Christian Bella amewapongeza wasanii mwenzake Alli Kiba na  mdogo wake Abdu Kiba kwa uamuzi waliouchukua wa kuoa.

Christian Bella amesema wasanii wengi hawapendi kuweka wazi mahusiano wao  hivyo ndoa si jambo jepesi kama wanafikiria mpaka unaona mtu ameoa basi ujue amefanya kitu kikubwa.

“Kuoa si kitu kidogo hasa wasanii maana ndio kunakuwa na changamoto mbalimbali ambazo usipokuwa makini unaweza kujikuta unaachana na mwenza wako.

“Nilipoletewa mualiko wa kuhudhulia kwenye sherehe ya Alli Kiba pamoja na kuimba nilifurahi sana kwani ni kitu cha heshima hata Mungu anakifurahia sana,” amesema Bella.

Sherehe ya ndoa ya wawili hao ilifanyika juzi katika ukumbi wa Hoteli ya Serena iliyopo Posta, Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wasanii mbalimbali akiwepo pia mke wa Rais mstaafu Mama Salma Kikwete.




Post a Comment

Previous Post Next Post