Mchungaji, Docho, ndo kwanza alikuwa ameanza
kumbatiza mfuasi wa kwanza kati ya themanini waliokwenda kufanyiwa huduma hiyo
katika ziwa Ayaba, huko Ethiopia wakati mamba aliporuka nje kutoka majini na
kumchukua mchungaji huyo.
Mchungaji alijitahidi kupambana na kujiokoa na
mashambulizi ya mamba huyo ambaye alikuwa amemsababishia majeraha makubwa.
Wakazi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na wavuvi walijaribu kutumia
nyavu ili kumuokoa na mamba huyo asimwingize kwenye kina kirefu ndani ya ziwa
hilo lakini hata hivyo juhudi zao hazikuweza kuokoa maisha ya mchungaji huyo na
walichoweza ni kuopoa mwili wake baada ya kuwa tayari amefariki.
Watu wanaoishi karibu na ziwa hilo katika mji wa
Arba Minch wanasema uvuvi uliopindukia umesababisha kupungua kwa chakula cha
mamba na matokeo yake mamba wamekuwa wakionekana wakiwinda kando kando ya Ziwa.
Chanzo:BBC Swahili
