Siku ya Alhamisi ya Tarehe 5 Julai mwaka huu moto utawaka dimbani kutokana na mminyano wa miamba ya soka nchi Yanga SC na Simba SC.
Watani hao wa jadi nchini watakutana kwenye kundi moja kundi (c) katika michuano ya Klabu Bingwa za Afirka na Mashariki na Kati (CECAFA) au Kagame Cup.
Kagame cup inatarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13 mwkaa huu Jijini Dar es Salaam.
Nicholas MusonyeKatibu wa kudumu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ametaja makundi kwenye mashindano hayo ameeleza licha watani wa jadi hao kuwa kwenye kundi moja lakini pia klabu Dakadaha ya Somalia na Saint George ya Ethiopia.
Kundi jengine ni A linalopambanisha klabu ya Azam FC, ya Tanzania, KCCA ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini
.Kundi B klabu ya Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti.

