Kila Klabu ina mkakati wake wa kujihakikishia unajisuka na kurejea vyema kwenye michuano ya msimu uja0 wa ligi kuu bara (VPL) na michuano mengine.
Klabu ya Simba tumeonda wametanga usajili wao kwa mchezaji Abdallah Salama, Rashidi Mo na wengine huku Azama wakiwasajili nyota wa yanga akiwa pamoja na Donald Ngoma na Juma Abdul
Klabu Yanga imekaa kimya bila kutangaqza majina ya wachezaji wao waliowasajili ambapo Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa amefunguka kuwa klabu hiyo haitangazi majina ya wachezaji wake kwa kuhofia kuibiwa .
Mkwasa ameeleza kuwa upo mchezo wa kuzidiana kete endapo ukitangaza majina ya wachezaji wako zipo Klabu zenye vitendo vya kuiba wachezaji.
Pamoja na kuwepo kwa tetesi za kusajiliwa kwa mchezaji mkongwo wa zamani katika klabu hiyo ambaye anakipiga Ndanda Mrisho Ngasa lakini Mkwasa anawasihi wanayanga kuwa na subira na kwamba watatangaza majina ya wachezaji watakao sajili kwenye wakati muafaka ambao sio sasa
Mkwasa amesikitishwa na hatua ya ukiukwaji wa kanuni za usajili kutokana na kutofungwa kwa dirisha dogo.
Amesema kuwa zipo timu zimekwenda kinyume na utaratibu huo "Unajua klabu zinazosajili hivi sasa zinaenda kinyume na utaratibu wa usajili, na hii yote ni kwasababu dirisha bado halijafunguliwa" amesema
