Bunge limeagiza Bodi ya Benki Kuu ya Tanzania-BoT na manejimenti
yake kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali-PAC kwa ajili ya
kujieleza kuhusu matumizi ya bima binafsi ya matibabu.
Agizo hilo lilitolewa jana bungeni jijini Dodoma, na Spika wa
Bunge, Job Ndugai ambapo alitoa muda wa wiki moja kwa bodi hiyo kufika mbele ya
kamati ya PAC.
Spika Ndugai alitoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck
Mlinga kudai kwamba BoT kuna ufisadi wa watumishi wake kuendelea kutibiwa nje
ya nchi.
Spika Ndugai aliagiza BoT, Mlinga na NHIF wakae kabla ya siku ya
Jumatatu.
Chanzo: Mwananchi
