Na. Aminah Kasheibar
Nguli wa muziki wa dansi, Johnson Nguza Viking 'Papii Kocha' amesema anatarajia kuoa hivi karibuni na mpenzi wake ambaye jina hakutaka lifahamike.
Papii Kocha amesema muda wa kuwa na familia umeshafika na hapo awali alikuwa anatamani sana kuoa.
Alisema kabla ya kuoa atambulisha mchumba wake kwenye jamii harafu maswala ya ndoa yatafuata.
"Nilikuwa natamani sana kuoa ila wakati wa kufunga ndoa umeshawadia ukizingatia nahitaji kuwa na familia na watoto.
"Kuoa ni jambo nzuri japokuwa wengi wa wasanii wapendi kufichua familia zao mimi nawapongeza wote wasioficha mahusiano yao," alisema
Hata hivyo Papii Kocha Alitoa fundisho na pongezi kwa wasanii wanaochipukia kuwa wasikate tamaa na muziki zaidi ya kuongeza ubunifu kwenye kazi.
