Hatua ya serikali ya Rais Donald Trump ya kuziwekea vikwazo
vya kiushuru bidhaa za chuma cha pua na bati, imewatibua washirika wa Marekani
ambapo Umoja wa Ulaya, Canada na Mexico zimeanza kulipa kisasi.
Mapema jana Juni mosi, 2018 Canada na Mexico zilitangaza
hatua za kujibu ushuru mpya uliowekwa na Marekani dhidi ya bidhaa hizo
zinazoingizwa nchini Marekani.
Wakati Canada na Mexico Zikitangaza uamuzi huo, Umoja wa
Ulaya-EU unasema uko tayari kujibu hatua hiyo ya Marekani iliyochochewa na Rais
Trump.
Ujerumani nayo haikuwa nyuma katika sakata hilo, ambapo
inasema nayo itashirikiana na Canada na Mexico katika kuratibu mkakati wa
pamoja dhidi ya Marekani. Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Fedha wa
Ujerumani, Peter Altmeier.
Nchi ya Ufaransa ambapo hivi karibu Rais wake, Emmanuel
Macron alizungumza na Trump katika mazungumzo hayo alimuonya rais huyo wa
Marekani kwamba amefanya makosa kuweka vikwazo hivyo na kwamba imefanya makosa.
Chanzo: D.W Swahili
