Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole ameonyesha
kushangazwa kwake na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe wa kutangaza ushirikiano wa vyama hivyo
katika usimamishaji mgombea kwenye jimbo la Buyungu.
Jimbo la Buyungu lililoko mkoani Kigoma, liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake,
Marehemu Kasuku Bilkago kufariki dunia siku kadhaa zilizopita.
Polepole ameeleza kuwa, hatua hiyo aliyoiita ya kugawana
ubunge imekiuka utamaduni wa kiafrika, na kwamba ilitakiwa wasubiri msiba wa
marehemu Bilago uishe ndipo watangaze hatua hiyo.
“Nimesikia jamaa palepale msibani walianza
kugawana ubunge na kuanza kujihadaa, ni bahati mbaya sana. Utamaduni wa
kiafrika ni kumaliza msiba ambapo lengo ni kufariji wafiwa. Nimekaa Kakonko kwa
muda wa kutosha, kwakuwa mmeanza siasa msibani, CCM tunasema wembe ni
uleule" amesema Polepole.

