Serikali imepoteza kiasi cha Sh. Trilioni 5.98 katika
kipindi cha mwaka 2009 hadi 2017, pamoja na kupata hasara ya trilioni 3.169 kwa
sababu ya mfumo mbovu katika sekta ya bahari kuu.
Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya
Bunge ya Ushauri wa Uvuvi wa Bahari Kuu, Anastazia Wambura wakati akizungumza
katika Makabidhiano ya taarifa za kamati maalumkuchunguza uvuvi wa bahari kuu
na gesi asilia.
Vile vile, Wambura amesema serikali imekuwa ikipoteza
bilioni 352 kila mwaka kupitia biashara ya usafirishaji samaki ghafi nje ya
nchi.
Amesema hasara hizo zimetokana na changamoto zilizopo katika
sekta ya uvuvi hali inayopelekea sekta hiyo kutotoa mchango mkubwa katika
ukuzaji wa uchumi wa nchi.
