Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza kuanza oparesheni ya kuwakamata na kuwatoza faini wachafuzi wa Mazingira kuanzia July 1, 2018 ili kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi.
Makonda amesema ameamua kufanya kwakuwa wakaz wa Dar es Salaam ni wachafu.
"Usafi ni moja ya tatizo kubwa katika jiji la Dar es Salaam, ni ukweli usiofichika kwamba Dar es Salam ni wachafu na wanatia aibu, tarehe 1 mwezi wa 7 tunaanza oparesheni ya usafi katika mkoa wangu," amesema
Amesema kuwa ameandaa vijana zaidi ya 4,000 kutoka Jeshi la kujenga Taifa JKT ambao watafanya kazi ya kuwakamata watupaji wa taka barabarani na mitaani.
Vijana hao 4,000 ni wale waliomaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi ambapo RC Makonda ameamua kuwachukuwa kwaajili ya kufanya kazi hiyo na kwenye kiasi cha faini watakazo watoza wachafuzi wa mazingira 40% itaenda kwa vijana hao na 60% itaingizwa serikalini.
Aidha Makonda amesema hawezi kukubali kuona jiji linakuwa kwenye hali ya uchafu wakati ipo sheria ya mwaka 2004 inayotoa mamlaka ya kuwawajibisha wananchi wenye tabia kuchafua mazingira kwa makusudi.
Itakumbukwa kila mwaka viongozi wamekuwa wakihimiza usafi na hata alipokuja Rais Barack Obama miaka kadhaa iliyopita barabara zilipigwa deki na alipoondoka uchafu ukaendelea na hivi karibuni Rais Magufuli alifanya usafi Kama sehemu ya kuhimiza usafi lakini bado watu wamekaidi, pia ulianzishwa utaratibu wa usafi kila jumamosi watu wasifungue maduka hadi wafanye usafi lakini bado pia wamekaidi jambo ambalo RC Makonda ameamua sasa kuja na mkakati wa kuwatumia vijana wa JKT wasiokuwa na kazi kufanya jukumu la kuwakamata wachafuzi wa mazingira.
