Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaotumia usafiri wa mabasi ya mwendokasi Jana, Juni 3 na leo Juni 4 2018 wamedai kusafiri kwa kutumia mabasi hayo bure.
Mmoja wa watumiaji wa usafiri huo Ngweshani ameeleza kuwa amefika kwenye kituo cha mwendokasi cha Kivukoni hakuona watumishi wa Udart wanakatisha tiketi wala wale wanahakiki tiketi kwenye mashine lakini watu wanasafiri.
"Nilivyouliza nikambiwa kuwa leo hakuna kulipa kusafiri ni bure basi nikaungana nao na nikapanda gari hiyo hadi mwisho wa safari yangu Mwanamboka kinondoni nako sikulipia"
Lucy Mushi amefika kwenye kituo cha mwendokasi cha Garezani karikakoo leo ambako hakuona watumishi wanaokatisha tiketi na gari zilikuwa zikiendelea na misafara ambapo yeye alikuwa akiwahi sehemua alilazimika kupanda busi iliyokuwa ikiienda Kimara bila malipo yoyote.
Juma Nambea naye ameeleza kuwa naye jana alitumia usafiri huo bila ya kulipa kiwango chochote cha fedha.
Inadaiwa kuwa watumishi wa Ofisi ya Udart zenye mamlaka na usafiri huo wale ambao wanahusika kwenye uaktaji wa tiketi wapo kwenye mgomo ambao hajafamika hadi sasa.
