Simba ,Yanga wakinukisha, washindwa kukaa hotel moja Kenya



Taharuki imeibuka baada ya Watani wa Jadi Simba naYanga  kukutana kwenye Hotel moja mjini Nakuru Nchini kenya waliwasili nchi humo kwa ajili ya mashindano ya ligi ya SportPesa.

Ni kwenye Hotel ya Midlands Hotel ambapo Simba imegoma kulala kwenye Hotel hiyo baada ya kuona na watani wao wamefikia hapo hapo.

Ikiwa imesalia siku moja kuanza kwa michuano hiyo Klabu hizo mbili za Tanzania zimeshindwa kukaa sehemu moja mpaka Simba wakatolewa kwenye hotel hiyo na kupelekwa sehemu nyengine.

Ligi hiyo itaanza Kesho Tarehe 3 Juni (Jumapili) ambapo Yanga wataminyana na Kakamega Home Boys kuanzia majira ya saa 7 kamili mchana huku JKU ya Zanzibar ikicheza na Gor Mahia FC saa 9 mchana.

Na Simba yenyewe itaanza Ligi Juni 4 Kesho kutwa (Jumatatu)  watakutana na klabu ya Kariobang Charks kuanzia majira ya saa 9 kamili mchana.

Post a Comment

Previous Post Next Post