Tundu
Lissu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), kesho Juni 4, 2018
atafanyiwa upasuaji wa 21 ambao ndio wa mwisho wa kuunga goti la mguu wake wa
kulia ambapo ataweza kutembea bila magongo.
Akiwataka
Watanzania wamuombea Lissu aliyekuwepo nchi ubelgiji anaweza kukunjua mguu wake
huu ulioathiriwa na shambulio la risasi alizopigwa Septemba 7 mwaka jana jijini
Dodoma.
Lissu kupitia ukurasa wake wa
mtandao wa picha wa Instagram leo Juni 3 akionekana amelala kwenye wodi huku
mkewe Alicia akiwa pembeni yake.
“Hello wapendwa wangu.
Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba Jumatatu Juni 4
nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia,” amesema.
“Ni operesheni kubwa
inayotazamiwa kuchukua takriban saa nane kwa taarifa nilizopewa tangu mwanzoni
mwa wiki hii. Hivyo madaktari wangu wametumia muda mrefu kidogo kuniandaa kwa
ajili ya Jumatatu.”
Ameeleza kuwa kwa sasa afya yake ipo vizuri na kwamba hiyo
ndio operesheni yake ya mwisho.
“Napenda niwajulishe kwamba ninajisikia vizuri
kiafya na baada ya kuwa kitandani tangu Aprili 11 (2018) nilipofanyiwa
operesheni ya pili, sasa niko tayari kwa ajili ya hii ya mwisho. Madaktari
wangu wako vizuri. Nina imani watafanya kazi nzuri ya kitabibu.”
Lissu alishawashukuru wote
waliomsaidia tangu aliposhambuliwa kwa risasi hadi sasa na kuwataka wazidi
kumuombea.
“Bado safari ni ndefu lakini
ninaweza kusema nimeanza kuona mwanga katika hili tanuru refu. Nimesema mara
nyingi kwamba ninaona fahari na faraja kwamba Watanzania wenzangu na wasio
Watanzania wamenitibu na wanaendelea kunitibu. Najua mtaniponya kwa nguvu za
Mola wetu na kwa upendo na ukarimu wenu. Nawaombeni msichoke. Nawashukuruni
sana,” amesema.

