Mahakama nchini Kenya imeamuru vigogo 24 walioshtakiwa
nchini humo kwa kosa la ufisadi na kula rushwa, wakae rumande kwa muda wa wiki
moja.
Watuhumiwa hao ni watumishi wa Shirika la Vijana wa Huduma
kwa Taifa Kenya-NYS akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Richard Ndubai na Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia,
Lilian Mbogo Omollo.
Mahakama imeamuru watuhumiwa hao wazuiliwe hadi siku ya
Jumatano ijayo ambapo uamuzi wa kuachiliwa kwa dhamana utatolewa.
Walikamatwa
na wengine wakajisalimisha kwa polisi Jumatatu wiki hii na kisha kufikishwa
kortini Milimani, Nairobi jana. Kikao cha kusikizwa kwa kesi dhidi yao
kiliendelea hadi usiku wa manane.
Chanzo:
BBC Swahili
