Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa
la Korea-KOICA na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani-WFP
jana Mei 29, 2018 yalikabidhi miradi 100 ya kijamii na programu ya Jumuiya za kukomesha
njaa kwa serikali ya Tanzania wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Kupitia programu hiyo,
washiriki kutoka vijiji vitatu walipata fursa ya kuimarisha njia zao za kujipatia
riziki kupitia vikundi vya ufugaji wakati ambapo zaidi ya miradi 100 ya jamii ilijengwa
au kukarabatiwa.
Miradi hiyo ilikuwa ni pamoja
na maghala, mifumo ya umwagiliaji maji, kutumia nishati ya jua, malamba na vituo
vya jamii. Miradi hii ilisaidia kuimarisha uwezo wa jamii kuhimili majanga kama
vile ukame na mafuriko na kutoa fursaza kiuchumi kwa washiriki katika kipindi
cha mwaka mzima.
Programu hiyo maarufu kama ‘Saemaul’
iliyogharimu Dola za Marekani milioni 5 imejengwa kwa kulinganisha na programu kama
hiyo iliyotekelezwa katikaJamhuri ya Korea miaka ya 1970, na ambayo ilitoa mchango
mkubwa katika kupunguza umaskini vijijini kwa kutumia miradi ya maendeleo iliyobuniwa
na kila jamii kwa kuzingatia mahitaji yao. Saemauli ina maana ya “kijijikipya”
katikalugha ya Korea.
Hafla hiyo ili fanyika katika
Kijiji cha Suli, Wilaya ya Chamwino, na kuhudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles
John Tizeba, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa, Aziza Mumba, Mkuu wa Wilaya ya
Chamwino,Vumilia Nyamoga, Mkurugenzi wa Nchi wa WFP Tanzania Michael Dunford, Naibu Mwakilishi wa
Nchi wa KOICA, Hyunsun Kim, Mkurugenzi wa Nchi wa shirikalisilo la kiserikali
la Good NeighboursTanzania, Namun Heo na wawakilishi kutoka tawala za mikoa.