Watanzania 11 walioshtakiwa kwa kosa la ubakaji nchini
Afrika Kusini wameachiwa huru na mahakama baada ya kukosekana kwa ushahidi.
Vijana hao mwaka jana walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Johannesburg kwa makosa ya kumteka nyara na kumbaka mwanamke mjamzito
ambaye ni raia wa Zimbabwe, Thelma Mondowa.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Johannesburg, Jaji Metisie
aliwaachia huru.
Kisa hicho kilitokea mnamo 15 Mei mwaka 2015 katika barabara ya
270 Lilian Ngoyi mjini Johannesburg, ambapo mahakama hiyo iliarifuwa kwamba
Mondowa alipata mkasa huo wakati akitoka kazini kwake na mfanyakazi mwenzake wa
kiume ndipo wakavamiwa na kundi la wanaume wenye silaha ambapo, lakini mwenzie
alifanikiwa kutoroka.
Wakili wa upande wa mashtaka wa serikali
alikuwa amemfahamisha hakimu kuwa Bi Thelma Mondowa aliamua kurejea Zimbabwe na
wameshindwa kupata anwani yake.
Chanzo: BBC Swahili
