Madee atamani Ramadhani isiishe kisa wasanii



Na. Aminah Kasheibar.

Staa wa muziki wa bongo fleva, Hamad Ally 'Madee' amesema atashangaa kuona msanii anafanya tamasha Katika mwezi mtufuku wa Ramadhani.

Madee amesema kwasasa wapo katika mwezi mtukufu hivyo inapaswa kusimamisha kazi zote za kimuziki na kufanya toba.

Alisema mwezi moja si miaka Mia ya kushindwa kufanya mema na kutubu kwa mbele ya Mungu kwa yale tunayoyafanya.

"Mwezi huu tunapaswa kusimama na kuomba dua ili tusamehewe kwa yale tuliyofanya ni jambo baya kuona msanii anafanya tamasha Katika ramadhani.

"Hata kuimba haistiri lakini hatuna jinsi Ni moja ya kazi ambayo inatupatia riziki ili familia zetu ziweze kupata mahitaji yao ya kila siku," alisema Madee.



Hata hivyo Madee amesema anatamani hata mwezi mtukufu usiishe kutokana na watu kuwa wastarabu na kuwa wanyenyekevu tofauti na miezi.

Post a Comment

Previous Post Next Post