Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdarahaman Kinana ameridhiwa rasmi ombi lake kujiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu wa hicho leo terehe 28 Mei, 2018, kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya chama hicho (NEC).
Wakati huo huo chama hicho kimetangaza wajumbe wapy wa NEC kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Katika Taarifa iliyotolewa Hamphrey Polepole katibu wa Itikadi na Uenezi ndani ya chama hicho ameeleza kuhusu kujiuzulu kwa Kinana.
"Napenda kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na CCM itaendeleaq kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadiri itakavyohitajika", imesema taarifa hiyo.


