Vita ya ufisadi nchini Kenya yapamba moto, Kigogo, maafisa watatu wadakwa na polisi


Polisi nchini Kenya wanawashikilia maafisa watatu waandamizi na Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa taifa-NYS, Richard Ndubai kwa tuhuma za ufisadi.

Hatua hiyo imekuja baada ya agizo la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma nchini humo, Nourdin Haji  la kuwataka watuhumiwa katika kashfa ya Sh. Bilioni 9 kushtakiwa.

Pia katika seke seke hilo, Washukiwa wengine kadhaa wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani katika kipindi cha saa 24, kulingana na afisa mmoja katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.
Pesa hizo zinadaiwa kuchukuliwa kutoka kwenye shirika hilo katika kipindi cha miaka mitatu, kwa mujibu wa duru mbali mbali.

Chanzo: BBC Swahili

Post a Comment

Previous Post Next Post