Mavunde afunguka mwanamke aliyevalia wigi kwenye nembo ya taifa


Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde amesema kuwa tuhuma za baadhi ya wabunge kusema kuwa nembo ya taifa inayotumika sasa haiakisi muonekano wa kitanzania sio kwamba nembo hiyo haiakisi bali ni moja ya alama ya taifa pia.
Mavunde amelieleza bunge jana kuhusu tuhuma hizo baada ya baadhi ya wabunge kuhoji uhalali wa Serikali kutumia nembo ya taifa ambayo picha zilizopo haziakisi uhalisia wa mwanamke wa kitanzania kwakuwa amevaa wigi.
“Maneno ya kwamba nembo yetu haiakisi muonekano wa kitanzania kwamadai kwamba mwanamke aliyepo amevaa wigi, sio kweli kwamba haiakisi na hii ni moja ya alama ya taifa,” amesema Mavunde.

Post a Comment

Previous Post Next Post