Z Anto awaahidi zawadi mashabiki zake

Nyota wa muziki wa bongo fleva Ally Mohamed  'Z  Anto' ametoa siri ya yeye kukaa kimya bila kutoa wimbo.

Z Anto ambaye alitamba na wimbo wa 'Binti kiziwi' ambao ulifanya vizuri kwenye stesheni mbalimbali za redio na televishini amesema alikuwa kimya kwasababu ya kuangalia soko là muziki lilivyokwenda na kujipanga ili aweze kukonga nyoyo za mashibi wake.

Alisema kipindi alipokuwa hasikiki kwenye vyombo vya stesheni alikuwa anaendelea na biashara nyingine huku akijapanga vema kwenye muziki.

"Nilikaa kimya kwaajili ya kujipanga ili nije kufanya vizuri kama hapo awali najua sasa soko la muziki linaushindi mkubwa zaidi bila juhudi hauwezi kutoka," alisema Z Anto.

Hata hivyo Z  Anto amesema baada ya mwezi wa Ramadhani kuisha ataachia wimbo wake kama zawadi kwa mashabiki wake.

Post a Comment

Previous Post Next Post