Baada ya kimya kirefu Shetta kuachia ngoma mpya Idd mosi



Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nurdin Bilal 'Shetta' amesema baada ya Sikukuu ya Idd ataachia nyimbo zake mbili.

Shetta ambaye kwasasa anatamba na wimbo 'Shikorobo' ambao unafanya vizuri kwenye stesheni mbalimbali.

Shetta amesema nyimbo zipo tayari ila muda wake wa kuziachia  bado kutokana na mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao unatakiwa kuheshimiwa na kutunukiwa.

Amesema mashabiki zake wasione kimya kwani Mambo yapo vizuri  kwaajili yao.

"Nimeshakamilisha nyimbo zangu ambazo natarajia kuzichia baada ya sikukuu ya Iddi kwasasa siwezi kuzitoa kutokana na mwezi wa Ramadhani ambao kwasisi waislamu tunatakiwa kusimamisha kazi zetu za kimuziki, " alisema Shetta.

Shetta amesema mashabiki zake waendelee kusapoti kazi anazozifanya kwa lengo la kukuza soko la muziki wa Tanzania.

Na Aminah Kasheibar

Post a Comment

Previous Post Next Post