Rais mstaafu wa Zimbabwe, Robert Mugabe amegoma kuitikia
wito wa bunge uliomtaka afike mbele ya kamati iliyoundwa kwa ajili ya
kuchunguza mapato ya madini ya almasi nchini humo.
Kamati ya Nishati na Madini nchini humo, imetaarifu kuwa
wito huo ulikuwa fursa ya mwisho kwa Mugabe kutoa utetezi wake mbele ya kamati
hiyo kuhusu tuhuma hizo kwa kujibu maswali yake.
Kiongozi wa kamati hiyo, Themba Mliswa alisema walimwandikia
barua ya wito Mugabe mara mbili, lakini hakuitikia wito huo.
Kamati hiyo imesema itatoa wito
wa mwisho kwa Mugabe ili afike mbele ya kamati hiyo Juni 11, 2018.
