Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka msanii Wema Sepetu
kuwasilisha mahakamani hapo nyaraka zinazothibitisha kupatiwa matibabu nchini
India.
Uamuzi huo wa mahakama umekuja baada ya Wema kushindwa
kufika mahakamani mara mbili mfululizo, ambapo imesema itatoa amri endapo
mshtakiwa huyo atashindwa kuwasilisha nyaraka hizo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ndiye
aliyetoa amri hiyo baada ya mdhamini wa
Wema ambaye ni mama yake mzazi, Mariam Sepetu kuwasilisha mahakamani hapo fomu
ya matibabu.
Baada ya mdhamini huyo kuwasilisha fomu, zilipingwa na
Wakili wa Serikali, Costatine Kalula kwa madai kuwa zilikuwa nyaraka za tiketi
za ndege.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13, 2018.
