Ikiwa zimepita siku mbili tangu
Dkt. Hellen Kijo-Bisimba kustaafu nafasi ya Ukurugenzi Mkuu katika Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu-LHRC,yameibuka madai mitandaoni kwamba Bisimba ameteuliwa
kuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee la Chadema.
Taarifa hizo zilisambaa leo Mei
30, 2018 katika mitandao ya kijamii hasa wa WhatsApp kupitia barua iliyodaiwa
kutolewa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene.
Mtandao huu ulimtafuta Makene kwa
njia ya simu kwa ajili ya kuthibitisha taarifa hizo, ambapo amekanusha kwamba
si za kweli. Barua hiyo inayodaiwa kuwa ni ya kughushi iko hapo chini.

