Yondani ahusishwa na mpango wa kutimka Yanga, Mzee Akilimali atoa povu


Baada kuwepo kwa taarifa ya kutoweka kwa Beki wa yanga Kelven Yondani na kuhusishwa kukacha kuchezea klabu hiyo Mzee wa Yanga Akilimali aeleza yamoyoni.
Yondani amemaliza Mkataba wake ndani ya Yanga na bado hajasaini Mkataba mpya hivyo hofu ya kusajiliwa na Klabu nyengine inatokana na hatua aliyoichukua leo ya kupotea bila kupatikana kwenye simu yake.

Mzee Akilimali amesema kuwa yeye ataangua chozi kutokana na kuondoka kwa mchezaji huyo kutokana na mchango wake ndani ya klabu hiyo.

Yondani amehusisha kukacha Yanga na kwenda kwa waramba Ice cream Azam Fc na huku ndiko atakapo saini mkataba mpya.

“Kama hizo taarifa ni za kweli Yondani ataondoka basi binafsi nitalia sana, sababu ni moja, kati ya wachezaji ambao walikuwa wanacheza kwa nguvu kubwa, alijituma bila kuan­galia klabu ipo kwenye hali gani basi ni Yondani.

“Waondoke wache­zaji wote lakini siyo yeye, itaniuma sana, siyo siri kwa jinsi ambavyo nam­fahamu mjukuu wangu, nimekuwa nikiongea naye mambo mengi kutokana na kuipenda timu na kujitu­ma,” alisema Akilimali.

Post a Comment

Previous Post Next Post