Lema-Kama ubaguzi utaondoka kwa viongozi Chadema kujiuzulu, tuko tayari kufanya hivyo


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kama ubaguzi wa rangi na vyama vya siasa nchini  utaondoka kwa viongozi wa Chadema kujiuzulu nyadhifa zao, wako tayari kufanya hivyo ili taifa libaki na mshikamano.

Lema ametoa kauli hiyo leo Mei 30, 2018 katika shughuli ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, Marehemu Kasuku Bilago.

Lema amesema kuwa, undugu na mshikamano katika taifa ni bora kuliko rangi na vyama vya siasa.


“Wabunge wa CCM wameondoka, unajiuliza tunaishi katika taifa gani ambalo ubaguzi unajengwa kwa rangi na vyama, kama ubaguzi huu utaweza kuondolewa kwa sisi kujiuzulu, nafasi zetu zote mpaka na mwenyekiti wa taifa, lakini taifa hili likabaki na mshikamano tutafanya hivyo hata kesho. Undugu ni bora kuliko rangi na vyama vya siasa,” amesema.

Post a Comment

Previous Post Next Post