Mhubiri anayefahamika kwa jina la Jesse Durplantis kutoka
nchini Marekani amewaomba waumini wake wamnunulie ndege yake ya nne.
Durlantis amesema Mungu amemwambia anunue ndege aina ya
Falcoln 7X inayogharimu dola milioni 54.
Mchungaji
huyo amesema awali alikuwa na shaka kuhusu kuendelea na ununuzi huo, lakini
Mungu alimwambia: "Sikukwambia uilipie. Nilikwambia uamini na
utaipata."
Akikazia
kuhusu dhamira yake hiyo, Durlantis amesema hata kama Yesu angekuwepo siku
hizi, asingepanda punda kama ilivyokuwa zamani.
Hatua
hiyo imeibua waumini wake na wadau wengine ambapo wamefananisha ombi hilo na
ulafi wa mali.
Watu
kwenye Twitter wamepokea ombi hilo kwa mshangao, wengi wakinukuu aya kwenye
Biblia zinazotahadharisha dhidi ya ulafi na "manabii wa uongo".
Wengine wanasema pesa hizo zingetumika vyema kuwasaidia maskini.
Chanzo:BBC
Swahili

Duuh!!! Ndege nne?
ReplyDeleteBalaa hili