Tshishimbi atajwa kunaswa na mtego wa Simba


Zipo dalili za wazi kuwa Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba inaiwinda saini ya kiungo machachari Papii Kabamba Tshishimbi yule wa Yanga

24SevenUpdater umedokezwa taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Simba kuwa tayari ipo mipango ya kumsajili kiungo huyo.

"Tshishimbi ni Midfider mzuri kuwahi kutokea hapa nchini lakini hajapata klabu nzuri itakayomfanya aonyeshe kiwango chake cha uchezaji".

Hata hivyo Tshishimbi amamaliza mkataba wa kiutumikia klabu ya yanga ingawa wanajangwani hao hawana nia ya kumuachilia kiungo huyo.



Haji Manara Msemaji wa Simba kwa mara ya kwanza amemsifia Tshishimbi licha ya kipindi cha nyuma kumuita 'Shilole' na kumbeza mchezaji huyo.

Cha kushangaza Manara ameeleza kuwa Tshishimbi ni Mchezaji wa kipekee ambaye hajapata nafasi ya kucheza angalau kwa nusu ya uwezo wake kutokana na Klabu aliyokuwepo.

Manara akimtakia kheri ya Siku ya kuzaliwa Tshishimbi alimwagia sifa na kuelewa kuwa anaheshimu kipaji chake.

Post a Comment

Previous Post Next Post