Hakuna ndoa ya uji -Sheikh mkuu Dar



Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amesema kuwa vijana wanaofunga ndoa siku chache kabla ya Mwezi Mktukufu wa Ramadhan (Shabani) ama mwanzoni mwa Mwezi Shaaban wasikejeliwe. 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisini kwake Sheikh Alhad amesema kuwa, ndoa hizo zisibezwe kwa kuziita ndoa za uji badala yake tuwaombee dua wanandoa hao.“Kwamba mtu amekaa kwa utukufu wa Ramadhan akaona hapana, siwezi kuendelea acha nifunge ndoa. Hii ni aina ya toba na kijana huyu ameamua kucha maasi-ameacha zinaa.
“Mtu ambaye amefanya hivyo, muombe kwa Mungu. Tusibeze hizo ndoa za namna hii kwamba tukuziita ndoa za uji … ndoa ni kitu kitukufu,” amesema Sheikh Alhad.
Amesema, heshima ya mwanadamu ni kufunga ndoa kabla ya tendo la ndoa “hawa vijana ambao wanaoa shaaban tuwaheshimu na tuwape moyo  kwamba, wanatafuta hifadhi na kujistili.”
 Amesema kuwa, mtu aliyefanya uamuzi huo hatuna budi kumuombea mwa Mwenyezi Mungu na kwamba, wengine wanaowa mwezi wa Shabaani kwa sababu ya kuchelewa kwa mipango yake ya ndoa hivyo huamua kuliendea suala hilo ndani ya Ramadhan

Post a Comment

Previous Post Next Post