Msanii wa Film nchi Sabrina Omary A.K.A Sabby Angel amefunmguka kuchukizwa na kauli ya aliyekuwa Mpenzi wake nyota wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba kuhusu yeye kutooa mwanamke wa Tanzania.
Sabby ameonyesha kuumizwa na kauli hiyo ilitolewa na Kiba ikiwa kwenye mahojiano na radio cha Clouds Radio na kueleza kuwa kauli hiyo ni ya dharau,
Wiki iliyopita Kiba alikuwa kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds alieleza sababu ya yeye kuwaacha warembo wote wa Bongo na kwenda kuoa Kenya ni kwa sababu wasichana wengi wakibongo wanaendekeza vigodoro na wengi sio wasomi.
Sabby Angel ameonekana kukasirishwa na kauli hiyo kutoka kwa mpenzi wake wa zamani na ameandika ujumbe huu: "Ni jambo la Kheri kwa Ali K kuoa lakini sijapenda comment yake eti kusema eti Tanzania hakuna wanawake wasomi wa kuoa.
"Binafsi kama mtu umeamua kuoa we oa tu kwa manufaa yako lakini sio kukashifu wanawake wote. Kwani hapo wakati anatoka na hao wanawake wa Kitanzania haukuona hayo mapungufu? Kwani watu wanaoa vyeti? Wanaoa kukimu mahitaji yao binafsi na kuzaana?.
"Hiyo ni kumaanisha hata wazazi wetu wa kike na hata mama yake ni wale wale it is very immature”. Ali Kiba alifunga ndoa na binti kutoka Mombasa Kenya wiki chache zilizopita
