Na Hamis Mguta, 24SevanUpdater
Katibu wa Itikati na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema wapo viongozi wa vyama vya upinzani wamekosa hoja za mashiko katika kufanya siasa na kujikita katika kusema uongo.
Polepole ameyasema hayo leo katika Ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Lumumba Kariakoo, Dar es Salaam akitoa hoja kuhusu taarifa iliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).
"Wapo viongozi wa upinzani baada ya kuona wamekosa hoja za mashiko za kufanyia siasa wamejikita na kubobea katika kusema uongo na kuupotosha ukweli, na wapo baadhi yao kwa kauli walizokuwa wakizisema kwa umma sisi kama chama hatuna tatizo na mtu kusema mambo hadharani kwasababu ni uhuru lakini tuna tatizo na mtu muongo,"
amesema Polepole.
Aidha amesema kuwa taarifa ya CAG kuwekwa hadharani ni utaratibu
mzuri ambao chama Cha Mapinzuzi
kimejiwekea na kimeielekeza serikali katika kuhakikisha ukweli na uwazi wa
shughuli za kiserikali.
"Baada ya taarifa ya CAG kuwasilishwa kwa rais hatukutaka
ibaki baki, tukasema ipelekwe hadharani, watanzania waone sisi kama taifa
tunakimbia kwa namna gani katika kuleta misingi ya utawala bora, kuna watu wanaomba kila jambo zuri la serikali lififishwe
hizi tabia ni za hovyo," amesema.
Kuhusu vyama vilivyobainika kuwa na hati chafu Polepole amesema kuwa vyama hivyo visiachwe hivihivi.
"Viko vyama vimetumia pesa zaidi ya milioni 700 bila kutoa hesabu unatumia kama pesa ya
mjomba wako hivi, unatumia hesabu hautoi, hawa wasiachwe hivihivi, viko vyama mifumo yake ya hesabu haifuati mifumo na vigezo
vya uhasibu wanatumia pesa mbichi hazipelekwi benki na wanafanya manunuzi
pasina kufuata taratibu za manunuzi.
"Kipo chama ambao wanatumia pesa mil 89 bila hesabu kibaya
zaidi Chadema milioni zaidi ya 520 hakuna hesabu unapopewa mkopo chama cha
siasa ukapokea pesa ni jukumu la mdhamini kufahamu, harafu bilioni zaidi ya
mbili pesa mbichi zinatumika juju," amesema.
Hata hivyo Polepole ameisifu taarifa ya CAG akidai kuwa ni nzuri.
