Vijana na Wakinamama 'wala shavu' Manispaa ya Ubungo



Na Hamis Mguta, 24SevenUpdater

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam, imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili mikopo ya Wakinamama na Vijana.

Hayo yamesemwa leo Jumatano 18/04/2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo  na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe Boniface Jacob wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano na benki ya CRDB ambapo mikopo hiyo itatolewa kupitia benki hiyo.

Meya Jacob amesema Halmashauri ya Manispaa imetenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ya mwaka mmoja nanusu waliyoitunza kwa uaminifu mkubwa ndio zikapatikana shilingi 1.9 Bilioni kwa ajili ya mikopo kwa kinamama na vijana.

Meya huyo ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo kwakuwa idadi yao imeonekana kuwa ndogo, ambapo pesa hizo zitakwenda nusu kwa vijana na nusu kwakinamama na 20% inakwenda kwa walemavu.


Kwa taarifa ya mratibu wa zoezi hilo, idadi ya Wanawake waliojitokeza  ni 11,321, vijana ikiwa ni 1124, ambapo kwa idadi hii ya vijana Mstahiki Meya ametoa wito kwa vijana kujitokeza zaidi na moja ya sifa ya kupata mkopo huo ni lazima mtu afungue akaunti crdb benki.

"Nikiwa Manispaa ya Kinondoni tuliweza kutenga 800M kwa ajili ya mikopo kama hii, lakini Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina muda wa mwaka mmoja na nusu tu lakini unaweza kuona kiasi tulichotenga kwa ajili ya mikopo kwa vijana na kinamama, ni kwa sababu tuko commited kuwasaidia wananchi wa Manispaa ya Kinondoni" amesema Meya Mhe Boniface Jacob.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Mhe John Kayombo na Muwakilishi aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Charles Kimei, Ndugu Philip Steven, Waheshimiwa Madiwani wa Ubungo na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Post a Comment

Previous Post Next Post