Na Mwandishi wetu, 24SevenUpdater
Mvua zilizonyesha mfululizo zimeharibu miundondombinu kwenye barabara ya inayounganisha kijiji cha Jimbo na Kilongwe na kisiwani Mafia na kusababisha kukwama kwa safari ndani ya kisiwa hicho kupitia barabara kuu ya Kilindoni.
Barabara hiyo kuu ya Kilindoni kwenda Bweni inayounganisha vijiji hivyo kwenye eneo la Daraja lilokuwa likifanyiwa ukarabati baada ya mvua hizo kuanza kunyesha.
Joseph Komba aliyekuwepo eneo hilo amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo umefanywa kwenye wakati ambao sio rafiki kutokana na mvua kuendelea kunyesha.
"Mkandarasi hakufanya kazi kwa uweledi kwani anajua wazi kuwa hiki ni kipindi cha mvua za masika"amesema Komba.
Makame Mwinyi mmoja wa wakazi wa Jimbo ameiambia 24SevenUpadater kuwa usafiri wa eneo kutika Kilindoni kwenda kwenye vijiji vya jimbo , Kanga na Bweni umekuwa wa shida.
Mwinyi amesema kuwa mtu analazima alipe shilingi 6,000 kwa kupanda gari kutoka Bweni hadi Jimbo eneo barabara ilipoharibika na kuvuka upande wa pili na kupanda gari hadi Kilindoni ambapo awali ilikuwa ni shilingi elfu tatu.
 
