"Nipo tayari kukamatwa, Kuuwawa"- Zitto Kabwe


Na Hamis Mguta, 24SevenUpdater

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa yupo tayari kukamatwa kwa kusema kuwa serikali ya awamu wa tano imeshindwa kuonyesha matumizi ya shilingi trilioni 1.5.

Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo ameyasema hayo kwa kuandika kupitia ukurasa wake wa Facebook akiapa na kukubali kukamatwa huku akieleza kuwa kuna mtu anashinikiza akamatwe kwa kutamka maneno hayo akielezwa kuwa amepotosha Umma.

"Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG. Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO.

"Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo (haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo (mawazo yangu hayatakufa) Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie," ameandika Zitto.

Post a Comment

Previous Post Next Post