Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza, Penny Mordaunt.
Mkutano huo ulifanyika jana Aprili 16, 2018 ambapo Makamu huyo wa Rais yupo nchini humo kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuia ya Madola (CHOGM) akimwakilisha Rais John Magufuli.
Katika mkutano huo Mama Samia alielezea hatua iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Elimu mara baada ya kuamua Elimu iwe bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Pia Makamu wa Rais alishukuru mradi wa DFID unatekelezwa mkoani Simiyu na kuomba mradi huo uongezewe maeneo ili uweze kuwanufanisha watoto wengi wa kike.
Pia alizungumzia namna majukwaa ya kuwawezesha wanawake kiuchumi yanavyofanya kazi huku taratibu mbalimbali zinafanyika ili mabenki yaweze toa mikopo kwa riba nafuu.
