Manispaa ya Ubungo yaweka historia


​​

Serikali kupitia Naibu Waziri wa ​Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda​ ​imeipongeza​ Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kuwa Halamshauri ​ya Kwanza na ya mfano kwa kutoa Fedha za Mikopo ya Wanawake na Vijana kwa asilimia 100​, kutoka katika Mapato ya Ndani.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Kakunda ameitaka Wizara ya ​TAMISEMI kuandikia Manispaa ya Ubungo barua ya pongezi​ kwakuwa jambo hilo limekuwa gumu sehemu nyingi na wengine kutenga fedha chache tofauti na Manispaa ya Ubungo ambao jana wamezindua zoezi la  ugawaji wa mikopo ya kiasi cha ​Tsh Billion 1.94​ ,wakati ina mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.


Naye ​Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface Jacob​ amesisitiza kuwa mikopo itatolewa kwa Vigezo bila kuangalia dini,kabila wala chama cha mtu.

​"Wanaosema Mikopo ni ilani ya CCM,wajiulize mbona kwingine kuna Halmashauri za CCM lakini hakuna mambo haya mazuri? Hivyo watu wajue viongozi  Makini na Imara wanatoka Chama cha Upinzani ndiyo Msingi na Chachu ya Mafanikio yetu"​

Halmashauri hiyo imeidhinisha kutoa fedha kwa Vikundi 364 ambapo vikundi 119 ni vya Vijana na Vikundi 245 ni vya wanawake huku jumla ya watakao nufaika na mikopo ni wananchi 11,312.

Post a Comment

Previous Post Next Post