Serikali yaikataa Barua ya kutaka Maaskafu KKKT wasalimu amri, Msajili asimamishwa


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Dr Mwigulu Nchemba amekanusha kuwa Serikali haikuwaandikia a Barua maaskofu wa kanisa la KKKT ya kuwataka wasalimu amri.

Dk. Nchemba amesema kuwa taarifa iliyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii haina ukweli wowote na kwamba wananchi wawe makini na matamko ya aina hiyo. " Nchi yetu ni moja na tunameweza kuishi siku zote kwa kuheshimiana japo tuna jamii na makabati mengi Tume weza kuishi kama ndugu,"Ameleeza.

 “Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo,” .

 Kadhalika, Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani. “Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali. 

Wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake.” Amesema. Pia Dk Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hivyo akawataka viongozi wa dini waendelee na kazi zao. Dk Nchemba amewataka viongozi wa dini kuendelea na kazi zao. 

“Nchi yetu ni moja na tunaishi kwa taratibu tulizojiwekea na tuna madhehebu mengi.” Amesema na kuongeza: “Wengine wameliona jambo hilo kama ajenda. Wananchi wawe makini, wasiwafuate watu hao wanaotaka kuwagawa.” 

Wakati huo huo Dk Nchemba amemsimisha kazi Msajili wa Taasisi wizara ya mambo ya ndani

Post a Comment

Previous Post Next Post