WARAMI waivaa CHADEMA kesi ya akina Mbowe



Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka (WARAMI), wamesema chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaingilia majukumu ya Mahakama.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti wa WARAMI, Philipo Mwakibinga amesema mkutano uliofanywa jana na viongozi wa CHADEMA ulijikita kushinikiza mahakama iwapatie kila wanachoamini wao kuwa ni sahihi.
“Viongozi wa Chadema jana wameongea na waandishi wa habari, mkutano wao wa jana ulishinikiza mahakama kuwapatia kile wanachokitaka wao, huku ni kuingilia uhuru wa mahakama”, amesema Mwakibinga.
Mwakibinga amewataka viongozi hao kuacha mara moja kutoa matamko yanayoonesha kuingilia mhimili wa mahakama, na kuiacha mahakama ifanye kazi zake bila kuingiliwa.
Katika hatua nyingine, WARAMI wamewataka viongozi wa dini nchini kuacha kutumika na wanasiasa, na badala yake wafanye majukumu yao ya kuhubiri neno la Mungu.
Wajumbe wa kamati kuu CHADEMA walizungumza jana kwenye mkutano wao na waandishi wa habari kuwa endapo viongozi wao wakuu wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi hawatapewa dhamani siku ya leo Machi 29, 2018, wataitisha mkutano wa kitaifa wa wabunge, madiwani, na wanachama wa chama hicho kujadili ni jinsi gani watawasaidia viongozi wao kupata dhamana.
Hata hivyo kilichotegemewa na viongozi hao kwa viongozi wao kupewa dhamana leo kimegonga mwamba baada ya Mahakama ya Kisutu Dar Es Salaam kuamuru Freeman Mbowe na wenzake kurudishgwa tena mahakamani Aprili 3, 2018, siku amba watasainiwa bondi ya Milioni 20 na wakiwa huru utaratibu wa ukataji wa rufaa utafanyika.

Post a Comment

Previous Post Next Post